Amri ya kutotoka nje usiku imetangazwa katika jimbo la Adamawa nchini Nigeria.
Jimbo hilo
limeungana na mengine mawili ya kaskazini mashariki ya, Borno na Yobe,
ambako serikali inasema kuwa wanajeshi wameanza oparesheni kubwa dhidi
ya wapiganaji wa kiislamu wa kundi la Boko Haram .
Rununu hazikuwa zifanya kazi katika baadhi ya sehemu za eneo hilo.
Maafisa wa serikali wameiambia BBC kuwa ndege za kivita huenda zikapelekwa katika oparesheni.
Walisema kuwa wanajeshi walishambulia sehemu za jimbo la Borno, ambako kundi la Boko Haram lina ngome zake.
Operesheni hiyo
inakuja baada ya serikali kutangaza hali ya hatari katika majimbo ya
Borno, Yobe na Adamawa Kaskazini Mashariki mwa nchi ambako watu 2,000
yatari wameuawa tangu mwaka 2009.
Amri ya kutotoka nje kuanzia saa za jioni hadi asubuhi imetangazwa katika jimbo la Adamawa ili kukabiliana na wanamgambo hao.
Mwandishi wa
BBC katika jimbo la Adamawa anasema kuwa uamuzi huo unashangaza kwani
hali ya usalama katika jimbo hilo sio mbaya ikilinganishwa na majimbo ya
Borno na Yobe.
Mnamo siku ya
Alhamisi wanajeshi walivamia kambi za wanamgambo katika mbuga ya wanyama
na ambayo inasifika kuwa moja ya ngome kuu za kundi la Boko Haram
Msemaji wa
jeshi la Nigeria Brigedia Generali Chris Olukolade, alisema kuwa
watatumia uwezo wao wote wa kijeshi kukabiliana vilivyo na wapiganaji wa
Boko Haram.
No comments:
Post a Comment