Pages

Sunday, 19 May 2013

MSIMAMO WALIGI KUU ENGLAND

Spurs fans look away now: The final table shows Arsenal ahead in the vital fourth spot

LIGI KUU ENGLAND: MSIMU WAISHA KWA MAGOLI KIBAO, ARSENAL, CHELSEA ZIPO LIGI YA MABINGWA!!

Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com, Soka In Bongo
SPURS KUCHEZA EUROPA LIGI!
SIR ALEX AAGWA KWA SARE YA 5-5 NA WBA!!
RVP ATWAA BUTI LA DHAHABU!!
BPL, Barclays Premier League, leo imemaliza Msimu wake wa 2012/13 kwa kukamilisha idadi ya Timu 4 za kucheza UCL,UEFA CHAMPIONZ LIGI, Msimu ujao kwa Chelsea na Arsenal kuungana na Mabingwa Manchester United na Manchester City na kuitupa Tottenham kucheza EUROPA LIGI.
Kabla ya Mechi za leo tayari alishapatikana Bingwa ambaye ni Man United na Mshindi wa Pili ni Man City na Timu zilizoshushwa Daraja ni Wigan, QPR na Reading.
Kilichobaki kilikuwa kinyang’anyiro cha Nafasi za 3,4 na 5 ambapo Chelsea imefanikiwa kukamata ya Pili na Arsenal ya 4 hivyo kucheza UCL lakini Chelsea, pamoja na Man United na City, zitacheza Makundi, na Arsenal kuanza hatua ya Raundi ya Mchujo na ikifuzu itaingia Makundi.
Tottenham, kwa kumaliza Nafasi ya 5, itacheza EUROPA LIGI kuanzia Hatua ya Mchujo.
Katika Mechi 10 za leo Jumla ya Mabao 36 yalifungwa huku Mechi ya mwisho kwa Sir AlexFerguson akiwa Meneja wa Man United kumalizika kwa sare ya Bao 5-5 walipocheza ugenini na West Bromwich Albion ambayo pia ilimuhakikishia Straika wao hatari Robin van Persie alieifungia Man United Bao moja hii leo akimaliza Msimu akiwa na Bao 26 na hivyo kunyakua Buti ya Dhahabu kwa kuwa Mfungaji Bora wa BPL Msimu huu.
Van Persie anafuatiwa na Luis Suarez wa Liverpool mwenye Bao 23 na Gareth Bale wa Tottenham mwenye Bao 21.
MATOKEO: Jumapili 19 Mei, Chelsea 2 Everton 1, Liverpool 1 QPR 0, Man City 2 Norwich 3, Newcastle 0 Arsenal 1, Southampton 1 Stoke 1, Swansea 0 Fulham 3, Tottenham 1 Sunderland 0, West Brom 5 Man United 5, West Ham 4 Reading 2 na Wigan 2 Aston Villa 2

No comments:

Post a Comment