Pages

Friday, 17 May 2013

EXCLUSIVE: SIMBA NA YANGA - BILA MILLIONI 100 HATUTAKI MECHI YETU IONYESHWE NA KITUO CHOCHOTE CHA TV

Wakati ikiwa imebaki siku moja kabla ya mtanange wa tani wa jadi Simba na Yanga kufanyika huku kukiwa na taarifa kwamba mchezo huo unaweza kuonyeshwa kwenye moja ya kituo cha TV, leo hii viongozi wa klabu hizo mbili wamezungumza exclusively na mtandao huu kuhusiana na mchezo wa timu zao kurushwa moja kwa moja na kituo chochote cha Television.

Awali shirikisho la soka nchini kwa pamoja na kituo cha SuperSport cha Afrika Kusini lilikuwa na utaratibu wa kile kilichoitwa SUPER WEEK ambapo baadhi ya mechi hizo zingeonyeshwa live kutoka Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Lengo la SuperSport la kuonyesha mechi hizo live ni ‘kuipromoti’ ligi ya Tanzania na wachezaji wake ili waweze kupata kuonekana na watu wengine na kuingia katika biashara nzuri ya soka.

Lakini viongozi wa vilabu vya ligi kuu waligoma mechi hizo kuonyeshwa bila wao kupata malipo hivyo mpango huo ukafa bila majibu ya kujitosheleza.

Lakini leo zimeibuka taarifa kwamba kituo hicho na shirikisho wapo katika hatua za kutaka mechi hiyo ya watani wa jadi ionyeshwe live.

Wakiongea na mtandao huu Ktibu Mkuu wa Simba Mtawala na makamu mwenyekiti wa Clement Sanga walisema: "Ikiwa kama  kama kuna mpango huo TFF wakae watambue kwamba hatutokubali mechi yetu ionyeshwe bure. Ni wakati sasa tupate kile tunachostahili sio kuwaingizia watu wengine fedha wasizostahili. Tamko letu la pamoja tunasema kwamba ikiwa kuna kituo chochote kinachotaka kurusha mechi yetu basi kitoe Millioni 100 - millioni 50 kwa kila timu na si vinginevyo. Ikiwa hakuna atakayeweza kufikia kulipa fedha hizo basi mechi yetu haitoonyeshwa na kituo chochote cha TV."

No comments:

Post a Comment