walikuwa wakisikia neno ‘Freemason’ ama ‘Illuminate’ kama inavyojulikana nchini
Kenya wengi walikuwa wanaiona ni habari kubwa, lakini kwa sasa hivi inaweza
kuchukuliwa kama sio big deal.
Sababu ni ile ile kuwa wengi wanaoendelea kwa haraka ama
kuwa juu katika kile wanachokifanya basi utasikia huyo ni member wa Freemason,
kwa upande wa Marekani wanasema ‘he/she just sold her/his soul to the
devil’. Japo kwa upande wa Marekani wapo
wanaokiri kufanya hivyo kweli, ila kwa Africa Mashariki hakuna msanii aliyewahi
kukiri.
Lakini yote hayo ni kama yanakanganya na kuonekana kama
hayana mantiki hasa pale ambapo vithibitisho vya kinachoongelewa huwa havileti
mantiki ya moja kwa moja. Pengine watu wanatafuta pesa kwa bidii na kumuomba
Mungu lakini kwa kuwa kwenye mstari wa juu wanajikuta wanahisiwa kuwa member wa
secret society (Freemason). Oh..au labda ndo vile kwa upande mwingine lisemalo
lipo na kama halipo laja !
Tunathubutu kuziita blaa blaa kwa upande mwingine, lakini
tukiweka kwenye mabano kuwa inaweza kuwa na ukweli, who knows!
Mtandao wa malimwengu wa nchini Kenya huenda ukawa na mfano
mzuri wa kile nilichokitaja hapo juu, mtandao huo kupitia mwandishi wake
imetaja majina ya wasanii wa Tanzania na Kenya wanaosemekana kuwa ni wafuasi wa
Freemason, lakini kizuri zaidi ni kwamba mtandao huo umejaribu kuonesha
vithibitisho na kushindwa kupata jibu la moja kwa moja kwa nini wasanii hawa
wamekumbwa na hili. Inabaki hivyo hivyo kuwa tetesi tu.
Nani anataja wenye wamejiunga na Illuminati? How does he/she know the artists are illuminati members, unless he/she is a member.
ReplyDelete