Pages

Sunday, 19 May 2013

LEJENDARI DAVID BECKHAM: AAGA KWA USHINDI NA MACHOZI JUU PARIS!

Proud: David Beckham was joined by his three sons with the Ligue 1 trophy after helping PSG to victory Upset: David Beckham applauded the fans as he left the pitch in tears after being substituted
Moving: The PSG players hugged Beckham as he was substituted
Na Baraka Mpenja wa msaada wa Sportsmail.com, Soka In Bongo
DAVID BECKHAM alitoka Uwanjani katika Mechi yake ya mwisho ya Nyumbani ya Klabu yake Paris St-Germain ambayo huenda ikawa ndio ya mwisho katika maisha yake ya Soka ya Miaka 20 huku akibubujikwa machozi.
Beckham, ambae alianza Mechi hiyo ya Ligi dhidi ya Brest kama Nahodha, alibadilishwa katika Dakika ya 81 na Mechi kusimama kwa muda huku Wachezaji wenzake wa PSG wakimshangilia na yeye akawa akitoka nje kwa machozi.
Mashabiki wengi wa PSG wamekuwa wakililia Beckham, Miaka 38, abakie kama Mchezaji badala ya kustaafu.
Msimu huu PSG ndio wamekuwa Mabingwa wa France na bado wana Mechi moja ya Ligi  Jumapili ijayo watakayocheza Ugenini na Lorient lakini inaaminika Beckham hatakuwepo.
Katika Mechi ya Jana PSG waliifunga Brest Bao 3-1 huku Beckham akitengeneza Bao moja kwa Kona yake kuunganishwa na Blaise Matuidi na Bao nyingine mbili kufungwa na Zlatan Ibrahimovic.
Bao la Brest lilifungwa na Charlison Benschop.
Mara baada ya Filimbi ya mwisho kwenye Mechi hiyo na Brest, Beckham aliwahutubia Mashabiki na kusema: “Nataka kumshukuru kila Mtu hapa Paris-Wachezaji wenzangu, Wafanyakazi na Mashabiki. Ni kitu kikubwa kumalizia Soka langu hapa. Nimemaliza Soka nikiwa Bingwa na kwenye Timu iliyonifanya nijione kama nimekaa Miaka 10!”
Wachezaji wa PSG walimbeba na kumrusharusha juu huku akishuhudia na Mkewe Victoria na Rais wa zamani wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy.

No comments:

Post a Comment