Pages

Sunday, 2 June 2013

BRAZIL VS ENGLAND KIVUMBI KUTIMKA LEO SAA NNE USIKU(22;00 PM)

Innocent: Luiz said that Neymar's comments were because he doesn't know much about EnglandPoor: England's last disappointing performance was in their 1-1 draw with the Republic of Ireland
BAADA kunusurika kufutwa, Mechi ya Timu za Taifa za Brazil na England itachezwa leo Usiku huko Mjini Rio De Janeiro kwenye Uwanja wa Maracana, ambao Jina lake rasmi ni Estadio Jornalista Mário Filho, ikiwa ni ufunguzi rasmi wa Uwanja huo uliofanyiwa ukarabati mkubwa.
Juzi, Jaji mmoja aliamua Mechi hiyo isichezwe baada ya Uwanja huo kutotimiza masharti ya usalama lakini baadae uamuzi huo ukafutwa baada ya Rufaa.
Tangu ufanyiwe ukarabati tayari Mechi moja ya maonyesho imeshachezwa iliyowahusisha Mastaa wa zamani wakati Manguli wa Brazil, Ronaldo na Bebeto, walipoongoza Timu tofauti hapo Aprili 27 na kushuhudiwa na Watazamaji Elfu 25.
Maracana, ambayo iliwahi kupakia Watazamaji hadi 200,000, ilijengwa kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 1950 ambayo Wenyeji Brazil walifungwa kwenye Fainali yake Bao 2-1 na Uruguay waliotwaa Ubingwa wa Dunia.
Kwa mara nyingine tena, Maracana itachezwa Fainali ya Kombe la Dunia hapo Mwaka 2014 wakati Brazil watakapokuwa Wenyeji na Uwanja huo utachukua Washabiki 78,838 wote wakiwa wamekaa Vitini.
Wakati huo huo beki wa Brazil na klabu ya Chelsea ya London, David Luiz amesema England hawana uwezo wa kutwaa kombe la dunia mwakani litakalofanyika nchini humo.
“England hawawezi kushinda kombe la dunia. Hawana mawazo hayo kwa sasa na itakuwa ngumu sana kwao”. alisema Luiz.
Luiz aliongeza kuwa “Niliwatazama kombe lililopita, hawakucheza vizuri, na mpaka sasa hawajabadilika hata kidogo”.
Nyota huyo ataitumikia timu ya taifa katika mchezo wa leo wa kirafiki dhidu ya england.

No comments:

Post a Comment